Flickr

Thursday 1 February 2024

Naomba Kuondoka Lyrics Video

Haya mapenzi namna gani?
Tunapigana mbele ya watoto jamani
Tunatusiantusiana mbele ya majirani
Mbona tunavuana mavazi hadharani
Najua kawaida binadamu zipo siku hawapatani
Lakini zogo letu halina mwisho kwa nini
Dhuluma dhuluma drama drama dhuluma ya nini
Kama mapenzi namna hii

Naomba kuondoka
Ayayaya
Naomba kuondoka
Ayayaya
Naomba kuondoka
Ayayaya
Naomba kuondoka
Ayayaya  

Haya mapenzi namna gani?
Mbona tunaishi kwama washukiwa kwa nyumba
Maneno yetu ni machungu kumbe yanashinda mimba
Usione nimenyamaza siku hizi sitaki kuchimba
Maisha magumu eh Mungu nirehemu nakuomba
Nikikumbuka tulipatana kanisani kichwa kinavimba
Najua walimwengu mtasema mengi kimeniramba
Kama mapenzi namna hii


Naomba kuondoka
Ayayaya
Naomba kuondoka
Ayayaya
Naomba kuondoka
Ayayaya
Naomba kuondoka
Ayayaya  


Ona sasa nimekung'oa jino
Ulitafuna vidole vyangu no no 
Makasisi wamenawa mikono
Tabia zetu aibu mno
Heri nkupe buriani mkono
Tusijeuana mukwano
Watoto wasijeteseka mu dunia ino
Haya mapenzi namna gani
Kama mapenzi namna hii


Naomba kuondoka
Ayayaya
Naomba kuondoka
Ayayaya
Naomba kuondoka
Ayayaya
Naomba kuondoka
Ayayaya  

0 comments:

Post a Comment